Swali hili linaonekana rahisi, lakini ndilo swali ambalo familia nyingi hulichelewa kuliza. Wengi huanza kusherehekea offer letter kabla hawajajua kama degree hiyo itatambulika Tanzania, kama professional body itaikubali, na kama course waliyochagua inaendana na kazi wanayotaka kufanya baada ya kurudi.
1. Jina la chuo pekee halitoshi
Chuo kinaweza kuwa maarufu, lakini bado course fulani ndani ya chuo hicho ikawa na changamoto kwa Tanzania. Ndiyo maana CMH haiangalii jina la university pekee. Tunaangalia institution, program, entry requirements, credits, curriculum, duration, na mode of learning.
2. TCU, NACTVET, na professional bodies vinaangalia vitu tofauti
Recognition ya academic qualification na professional licensing si kitu kimoja. Mwanafunzi anaweza kuwa na degree ambayo inaonekana sawa kitaaluma, lakini ikashindwa kumpa professional registration kwenye field kama medicine, engineering, pharmacy, law, au nursing. Kwa hiyo verification inapaswa kuangalia njia nzima ya career, si admission tu.
3. Mode ya masomo inaweza kubadili matokeo
Online, distance, blended, campus-based, na part-time learning zinaweza kutazamwa tofauti wakati wa equivalence. Kabla ya kuchagua program, ni muhimu kujua kama mode ya masomo inakubalika kwa level yako na professional goal yako. Usisubiri hadi graduation ndipo uanze kuuliza.
4. Transcript yako pia inalindwa mapema
Hata kama chuo na course viko sawa, uchaguzi wa subjects, electives, credits, internships, na clinical/practical hours unaweza kuathiri equivalence. Hapa ndipo protected study plan inakuwa muhimu. CMH humsaidia mwanafunzi kujua vitu ambavyo havipaswi kuachwa wakati wa masomo.
5. Jibu sahihi linahitaji check ya case yako binafsi
Hakuna jibu moja kwa kila mtu. Course inaweza kuwa nzuri kwa mtu mmoja na ikawa risk kwa mwingine kulingana na career target yake. Ndiyo maana CMH huanza na consultation na equivalence risk review kabla ya recommendation ya mwisho.
Una course au chuo tayari?
CMH inaweza kukagua recognition risk kabla hujalipa application fee, tuition, au kusafiri.